The House of Favourite Newspapers

Fei Toto: Hawa Azam Ndio Nawataka

0

KIUNGO mchezeshaji fundi kipenzi cha mashabiki wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amesema mechi ngumu dhidi ya Simba na Azam FC ndizo anazozitaka.

 

Kauli hiyo ameitoa wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa leo Jumamosi saa moja usiku Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kiungo huyo hadi hivi sasa amefanikiwa kufunga mabao mawili huku akipiga asisti moja katika michezo mitatu ya ligi.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Fei Toto alisema kwake mechi ngumu ni zile dhidi ya timu ndogo kama vile Biashara United, Mbeya Kwanza na nyingine akini siyo Simba na Azam watakaocheza nao kesho.

Fei Toto alisema binafsi kwake amejiandaa vema kwa ajili ya kuvaana na Azam huku akiwa na matumaini ya ushindi katika mchezo huo.


Aliongeza kuwa anaamini
Azam wataingia uwanjani wakiwa wamepania, lakini kwake atatulia akifanya majukumu yake ya kuchezesha timu, kutengeneza nafasi na kufunga ndani ya wakati mmoja.


“Timu kubwa kama hizi
za Simba na Azam presha inakuwepo kwa mashabiki pekee lakini siyo kwetu wachezaji. “Kama mimi kwangu hakuna mechi rahisi kama tukicheza dhidi ya Simba na Azam, ninacheza kwa kujiamini kupitiliza kutokana na kuwajua baadhi ya wachezaji.


“Lakini hizi timu ndogo
ngumu kwanza kuwajua wachezaji wao na aina yao ya uchezaji, hivyo kuelekea mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam tumejiandaa vema kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Fei Toto.

Leave A Reply