The House of Favourite Newspapers

Shahidi Achanganya Mambo Kesi ya Mbowe – Video

0

NI Oktoba 29, 2021 kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Division ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi ushahidi wa Upande wa Jamhuri katik kesi no 16/2021 umeendelea ambapo shahidi namba tatu kati ya mashahidi 24 wa Jamhuri ameanza kutoa ushahidi wake.

 

Ilikuwa hivi, majira ya saa 3:50 asubuhi Jaji wa Mahakama Kuu, Joachim Tiganga ameingia mahakamani kwa ajili ya muendelezo wa kesi hito inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu.

 

Akiongozwa na na wakili mwandamizi wa serikali Pius Hilla shahidi no 3 ambaye anafanya kazi katika maabara ya Uchunguzi wa kisayansi, kitengo cha uchunguzi wa silaha na milipuko, afisa polisi No F5914 Coplo Khafidh Abdallah ameieleza mahakama namna ambavyo.

 

Sehemu ya maswali hayo, Koplo Hafidhi akiulizwa na wakili wa upande wa utetezi, John Mallya.

MALLYA: Kwenye ripoti yako umesema hapa kuna errors. Je kuna errors ngapi?
KOPLO HAFIDH: Hiyo hiyo moja.
MALLYA: moja inakua error au errors?
KOPLO: Inategemea.
MALLYA: Maana ya terrorist ni nini?
KOPLO: Ni ugaidi.
MALLYA: Na Terrorism maana yake nini?
KOPLO: Ni masuala ya utalii. (Mahakama inaangua kicheko)
MALLYA: Narudia tena. Terrorist umesema ni Ugaidi sio?
KOPLO: Ndio.
MALLYA: Na terrorism maana yake nini?
KOPLO: Ni masuala ya utalii.
Mahakama inaangua kicheko, hadi Jaji anashindwa kujizuia.!

 

Aidha, Kopleo Hafidhi ameieleza mahakama kuwa, Novemba 25, 2020 alivyopokea vielelezo kutoka ofis ya DCI alivyokabidhiwa na Gudluck ambapo alipokea Pistol no A5340 yenye magazine pmoja na risas 3 zilizoambatanishwa na barua iliyoeleza kuwa zilitakiwa kufanyiwa uchunguzi kama ni nzima au laah!

 

Full video kuhusu kilichotokea mahakamani ipo #GlobalTVOnline

Leave A Reply