The House of Favourite Newspapers

Fid Q na Maurice Ndani ya Coke Studio Leo

0

Msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva Fid-Q akikamua.

Baada ya wasanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba kutoka Tanzania na Victoria Kimani kutoka Kenya wiki iliyopita kumwaga raha ya burudani kupitia onyesho la muziki la Coke studio linalorushwa na luninga ya Clouds kila siku ya Jumamosi. Leo nyota wengine wa muziki huo Fid Q kutoka Tanzania na Maurice Kirya kutoka nchini Uganda watawasha moto.

Wasanii hawa wawili ambao wanatamba kwa muziki wa Bongo Fleva katika ukanda huu wa Afrika Mashariki wamefanya Kolabo matata (Mash-up) katika msimu huu wa Coke Studio unaoendelea.

Wasanii wengine kutoka Tanzania waliopo kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio mwaka huu ni Ben Pol ambaye alifanya kolabo matata(mash-up) pamoja na mwanamuziki nguli kutoka Kenya anayejulikana kama Wangechi, , Vanessa Mdee amefanya kolabo matata(mash-up) na mwanamuziki nguli kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kama 2Face,na Ali Kiba ameshirikiana na Victoria Kimani.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa onyesho hili hivi karibuni Meneja wa Bidhaa za Coca-Cola Nchini Maurice Njowoka alisema kuwa wasanii nguli kutoka Tanzania wanaungana na wasanii wengine 27 barani Afrika katika msimu wa tatu wa maonyesho ya burudani ya muziki maarufu kwa jina la Coke Studio Afrika ambalo linaendelea kuonyeshwa katika nchi mbalimbali.

Alisema kolabo ya wasanii 55 itashirikisha wasanii wawili kutoka nchi mbili tofauti kuimba nyimbo mbili za mitindo tofauti. “Mtindo wa Kolabo (Mash –up) uliwahi kutumika hapo awali katika maonyesho ya televisheni,sinema na wakati wa kupiga muziki mchanganyiko lakini safari hii unatumika katika onyesho la Coke Studio na utawawezesha wasanii watakaoshiriki kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika kuwa wabunifu na kuboresha viwango vyao vya sauti za uimbaji”.Alisema

Leave A Reply