The House of Favourite Newspapers

Filamu za Global TV mubashara kwenye simu

Magreth.

IKIWA imesalia wiki moja kufungwa kwa kura za msimu wa pili wa Tuzo za Sinema Zetu nchini zijulikanazo kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF), filamu kutoka Global TV Online ambazo zimeingia katika tuzo hizo, Ardhi ya Damu, Chanzo Ni Wewe na Coretha zinaendelea kuruka mubashara ‘live’ kwenye simu za mkononi.

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART ONE)

 

Akizungumza na Star Showbiz, mmoja wa washiriki wa filamu hizo kupitia Filamu ya Ardhi ya Damu, Sango Johannes alisema mwisho wa mwezi huu ndiyo utakuwa kilele cha kufungwa kwa kura hivyo watazamaji na wadau wa filamu waendelee kuzitazama filamu hizo zinazoendelea kuruka Global TV Online.

 

Maseke

“Tunashukuru kwa filamu zetu tatu kupokelewa vizuri katika Tuzo za Sziff kwani tunapata simu nyingi kwa wasomaji na wafuatiliaji wa filamu za Coretha, Ardhi ya Damu na Chanzo ni Wewe, kikubwa tuendelee kuwa pamoja hadi mwisho wa kufungwa kwa kupiga kura,” alisema Johannes.

GLOBAL MOVIES: CHANZO NI WEWE (PART TWO)

 

Filamu hizo zinaruka kila siku ya Jumamosi kupitia Global TV Online na unachotakiwa ili uweze kuwa mwanafamilia, ingia katika Mtandao wa Youtube kisha tafuta Global TV Online na baada ya hapo bonyeza neno Subcribe bila kusahau kengele ya pembeni yake ili uwe unajulishwa kila ikiwekwa.

Rhoida

Filamu zilizoingia katika tuzo hizo ni Ardhi ya Damu, Coretha na Chanzo ni Wewe. Jinsi ya kupiga kura, ingia sehemu ya kuandika meseji kwenye simu yako;

 

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART ONE)

 

Kwa Msanii Bora wa Kiume, andika BM kisha acha nafasi andika 1000, acha nafasi kisha andika *8 na utume kwenda namba 0683 520006 utakuwa umempigia kura Emmanuel Maasa aliyecheza Filamu ya Coretha.

Msanii Bora wa Kike, Rhoida andika BF acha nafasi kisha andika 760, acha nafasi andika *9 kisha tuma kwenda namba 0683 520006.

Surej

Kupigia kura Filamu Bora ya Mwaka kupitia Filamu ya Ardhi ya Damu andika 760 kisha acha nafasi, andika *9 na tuma kwenda 0683 520006.

Filamu ya Chanzo Ni Wewe andika 360 kisha cha nafasi, andika *7 na utume kwenda 0683 520006.

Filamu ya Coretha andika 1000 kisha acha nafasi, andika *8 na utume kwenda 0683 520006.

 

GLOBAL MOVIES: CORETHA (PART TWO)

Tuzo hizo za SZIFF ambazo huandaliwa na kituo cha TV cha Azam kupitia chaneli yao ya Sinema Zetu, pazia la kupiga kura linatarajiwa kuhitimishwa Januari 31 na tuzo zenyewe zikitarajiwa kutolewa Februari 23, mwaka huu.

Comments are closed.