The House of Favourite Newspapers

First 11 Ya Yanga Vs Simba Hii Hapa

Kikosi cha timu ya Yanga.

Leo Jumamosi, Yanga ikitarajiwa kupambana na Simba, tayari kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera ameshapata kikosi cha kwanza kitakachoanza katika mchezo huo.

 

Yanga ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 58, itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Kikosi cha Yanga ambacho kimepiga kambi mkoani hapa tangu Jumatatu ya wiki hii, kime­kuwa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia uliopo Bigwa.

 

Katika mazoezi ya jana asub­uhi, Zahera raia wa DR Congo, alionekana kuwa makini na kikosi ambacho kinaaminika ndicho kitaanza katika mchezo huo wa kesho.

 

Kikosi hicho kilikuwa kinaun­dwa na Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey ‘Boxer’, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mrisho Ngassa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Heritier Makambo, Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu.

 

Zahera aliwagawa wache­zaji wake kwenye vikosi viwili ambapo kikosi hicho wachezaji wake ndiyo walionekana kuwa ndiyo wana nafasi kubwa ya kuanza.

Comments are closed.