The House of Favourite Newspapers

Fiston Aanza Mazungumzo na Klabu Tatu

0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Abdoul Razack ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, tayari ameanza mazungumzo na klabu tatu tofauti ambazo zimeonyesha nia ya kuhitaji saini yake.

 

Fiston aliyejiunga na Yanga Januari, mwaka huu, mkataba wake na Yanga umebaki takribani miezi miwili kabla ya kumalizika.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Fiston aliyefunga bao moja kwenye ligi kuu na FA moja, alisema: “Kila mtu anaweza kuwa anajiuliza je, nimeongezewa mkataba au hatima yangu itakuwaje bila kutaka kujua je, ikinibidi kuongeza mkataba nipo tayari?

 

“Ndio, nipo kwenye mazungumzo na klabu zaidi ya tatu na tukifikia makubaliano mtazijua, pia sihitaji kuulizwa maswali kuhusu mkataba, ngoja niweke akili yangu kwenye mechi zilizobaki, bado tuna kazi ngumu ya kupigania ubingwa.”

STORI; CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave A Reply