The House of Favourite Newspapers

Fiston Apigwa Mkwara Mzito…

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ameonyesha hataki mchezo ndani ya kikosi hicho kufuatia kuwataka nyota wote wa kikosi hicho akiwemo Saido Ntibazonkiza ‘Saido’ na Fiston Abdulrazak kuhakikisha wanaulinda uzito waliokuwa nao.

 

Wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya siku 10 hadi tarehe 25 ndipo kikosi kitarejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya ligi inayotarajia kuendelea Februari, mwaka huu.

Taarifa ambazo Championi Jumatano, imezipata kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa, benchi la ufundi la timu hiyo limewapima uzito nyota wote kabla ya kwenda mapumziko mafupi na iwapo mchezaji yeyote atarudi na uzito tofauti na ule alioondoka nao basi atapigwa faini kutokana na kutozingatia programu aliyopewa na kocha.

 

“Kocha amezungumza na wachezaji na amewataka kuhakikisha kila mmoja anakuwa makini kwa kuzingatia uzito wake kwa kuhakikisha hawali vitu vyenye sukari nyingi pamoja na vyenye protini nyingi ili kuhakikisha wanakuwa katika uzito ule anaoutaka kocha ikiwa ni pamoja na kuendeleza mazoezi amesema kama mchezaji akizidisha uzito atapigwa faini,” alisema mtoa taarifa huyo.

Stori: Khadija mngwai, Dar es Salaam

Leave A Reply