Fitna Zawaondoa Yanga SC Klabu Bingwa Afrika

KWA walichowafanyia Yanga unaweza kusema kuwa Wanaijeria sio watu wazuri kwa kuwa wametumia nguvu kubwa kuwatoa mchezoni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Licha ya kutolewa katika hatua za awali kwa jumla ya mabao 2-0, Yanga walifanyiwa figisu za kutosha nchini Nigeria na waliingia uwanjani wakiwa wamechoshwa na mizingwe ya wenyeji hao.

 

Jitihada za wachezaji wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ziligonga mwamba Uwanja wa Andokiye Port Harcourt nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara alisema kuwa walipewa majibu rasmi kuhusu Virusi vya Corona dakika 45 kabla ya mchezo kuanza.

 

“Dakika 45 kabla ya mechi kuanza tumeletewa majibu kuhusu Corona ndio Yanga inapewa majibu, haijawahi kutokea, majibu yamekuja ya kihuni, huu mpira unaendeshwa kihuni,” alisema Manara.

 

Kwa kupoteza mchezo huo Yanga inatarajiwa kutua nchini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25 ikiwa ni kwa ajili ya ufunguzi wa ligi.

 

Kwa mujibu wa Yanga imeelezwa kuwa kuna wachezaji wanne ambao ni Feisal Salum, Yacouba Songne, Djigui Diarra na Mukoko Tonombe walitajwa kuwa na Corona jambo lililowatoa mchezoni.

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

 


Toa comment