The House of Favourite Newspapers

Usichojua Kuhusu Msanii Mpya Wa Rayvanny

0

 

MKURUGENZI wa lebo ya muziki ya Next Level Music (NLM) ambaye pia ni msanii aliye chini ya Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Rayvanny amemtambulisha msanii wake wa kwanza kuanza kufanya naye kazi chini ya lebo yake hiyo ambapo kila mtu ametaka kujua msanii huyo ni nani hasa?

Rayvanny amemtambulisha msanii huyo aitwaye Mac Voice kuwa msanii wa kwanza ambaye ataanza kusimamiwa kazi na lebo hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny au Chui ameposti kionjo cha kumkaribisha msanii huyo na kuandika; “Mtoto wa kwanza wa Next Level Music @macvoice_tz . Karibu kwenye familia kubwa…”

Rayvanny au Chui alimalizia kwa kuandika tarehe 24/9/2021.

Kwa wasiomjua, Mac Voice siyo msanii mgeni machoni kwa wapenda burudani nchini Tanzania kwani awali alishafanya kazi chini ya msanii Chege Chigunda na kufanikiwa kuachia nyimbo mbalimbali kama Teamo Remix na Bamba ambazo zinaendelea kufanya vizuri.

STORI: RICHARD BUKOS, DAR

Leave A Reply