The House of Favourite Newspapers

FLASH ‘Yamtoa Jasho’ JPM, Asachi Koti, Suruali Lakini Wapi – Video

KITUNZA data aina ya (Flash Disk) chenye orodha ya majina ya wafanyabiashara wakwepao kodi imeibua gumzo Ikulu baada ya Rais John  Magufuli  kujikagua kila kona ya mifuko ya nguo aliyoivaa bila kuiona.

 

Magufuli leo Juni 7, amekutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wakubwa 1,000 kutoka wilaya zote 139 nchi nzima, Ikulu jijini Dar es Salaam na kusema kuwa changamoto za ukwamishaji wa biashara kwa upande wa serikali ni kutokana na utitiri wa taasisi za udhibiti.

 

Aidha, ameongeza kuwa zipo taasisi nyingi za udhibiti ambazo zinaingiliana kimajukumu, kwa  mfano TBS, NEMC, WAKALA WA VIPIMO, TUME YA USHINDANI, EWURA, SUMATRA, TFDA, OSHA, OFISI YA MKEMIA MKUU, Na kadhalika.

TAZAMA TUKIO ZIMA HAPA

Comments are closed.