The House of Favourite Newspapers

Flaviana Matata Agawa Taulo za Kike Z’bar

0

 

MWANAMITINDO na mfanyabiashara Flaviana Matata Mei 28 alifika visiwani Zanzibar ,  ikiwa ni siku ya hedhi duniani ametumia nafasi hiyo kugawa taulo za kike aina ya (Lavy Pads) wakishirikiana na Marie Stopes ambao walitoa elimu ya namna gani wasichana na wanawake wanapata elimu juu hedhi salama.

Hatuwatengi na hata Marie Stopes wakiwa wanatoa elimu ya hedhi salama hatuwatengi, tukiwatenga wasichana tutaendeleza dhana potofu watoto wanakuwa hawana elimu ya hedhi salama,hata mabinti ukiwauliza wanakuwa na ukakasi  amesema Flaviana.

 

Kauli mbiu ya mwaka 2021 wanawake na wasichana kupata hedhi salama, zoezi la ugawaji wa pad liliendana sambamba na utoaji elimu kutoka Marie Stopes juu ya hedhi salama kwa wanawake ,jumla ya wasichana 270 walipata pad bure aina Lavy Pads.

 

Leave A Reply