The House of Favourite Newspapers

Flora, Riyama wafunikana kukata nyonga ukumbini

0

MAHARIYAFLORAMVUNGI11.jpgFlora Mvungi.

Na Musa Mateja

STAA wa filamu Bongo, Flora Mvungi na shostito wake, Riyama Ally juzikati walijikuta wakigeuka kivutio ukumbini baada ya kufunikana kwa kuzikata nyonga bila aibu kwenye hafla ya kumpongeza mtoto wa Flora, Tanzanite Hamis kuchaguliwa kuwa balozi wa duka la kuuza nguo.

Riyama3.jpgTukio hilo lilitokea hivi karibuni Hoteli ya City Style Sinza-Mugabe jijini Dar es Salaam, ambapo wawili hao walivamia katikati ya ukumbi na kuanza kushindana kuzungusha nyonga hadi kufikia hatua ya kuacha kucheza wakiwa wamesimama na kuamua kulala chini.

“Jamani huyu si Riyama na yule aliyelala ni Flora, mhhh wanajua kuzikata,” ilisikika sauti ya mhudhuriaji ukumbini hapo.

Leave A Reply