The House of Favourite Newspapers

FM Academia kulirudisha sebene kivingine

0

fm academia-wazee -official imageWAKONGWE wa Muziki wa Dansi, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ chini ya Prezidaa Nyosh El Saadat wanatarajiwa kulirudisha sebene kivingine Agosti 12, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hisaje Park, Boko jijini Dar.

Akizungumza na Showbiz prezidaa wa bendi hiyo, Nyosh Eld Saadat alisema kuwa usiku huo utakuwa wa aina yake kutokana na kuwepo kwa burudani mwanzo mwisho.

“Tutatambulisha staili mupya na sebene la aina mupya, niwaombe mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia makamuzi ambayo hayajawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa bendi hii,” alisema Nyosh.

Mbali na FM Academia, Yamoto Band pia wataku-wepo usiku huo ambapo watapiga nyimbo zao zote kali huku wakizindua nyimbo zao mbili, Suu na Mijudo kwa mara ya kwanza ndani ya ukumbi huo.

Leave A Reply