MWILI wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, marehemu Ruge Mutahaba umeagwa katika ibada maalum iliyofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Bukoba mkoani Kagera.
Viongozi mbalimbali wamejitokeza kuaga mwili wa Ruge wakiwemo Mawaziri, wabunge, viongozi wa vyama, dini, wasanii, ambao kwa pamoja wameungana na ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa Bukoba kuusindikiza mwili wa Ruge katika nyumba yake ya milele.
Baada ya shughuli za kuaga mwili wa marehemu Ruge Mutahaba kumalizika katika viwanja vya Gymkhana, tayari safari ya kuelekea Kijijini kwao Kiziru-Kabale kwaajili ya maziko imeanza.
Comments are closed.