The House of Favourite Newspapers

PRINCE STATIONERY WAJA NA OFA YA PUNGUZO VIFAA VYA MAOFISINI

Prince Stationery, wauzaji bingwa wa vifaa vya maofisini na shuleni kwa jumla na rejareja, wametangaza ofa kubwa katika msimu huu wa mwanzo wa mwaka, kwa makampuni, taasisi, mashirika na watu binafsi, wanaohitaji vifaa vya maofisini.

 

Akizungumza na Ijumaa, Meneja Mkuu wa Prince Stationery, Abdul Aziz Khatib, amesema wanatoa punguzo kubwa kwenye maduka yao yaliyopo Kariakoo, Mtaa wa Lindi karibu na msikiti na Mtaa wa Kongo kwa wote wanaohitaji vifaa vya maofisini, ikiwemo vifaa vyote vya stationery kama mafaili, karatasi nyeupe (rims), notebooks, diary, ink pads, mashine za kukatia karatasi, kuweka lamination na kadhalika.

“Vifaa vyote muhimu kwa maofisi vinapatikana kwenye maduka yetu kwa bei nafuu sana. Na uzuri ni kwamba bidhaa zetu ni za ubora wa kiwango cha juu, mteja akija lazima mwenyewe ataridhika na kesho atarudi tena, tunajiamini katika hilo,” alisema Abdul Aziz.

 

Akaongeza kwamba, mbali na kutoa huduma kwenye maduka yao mawili yaliyopo Kariakoo, Plot Number 12, Block 4, Mtaa wa Lindi jirani na msikiti, na duka lingine lililopo Mtaa wa Kongo, wanao uwezo wa kuwahudumia wateja hata waliopo mikoani, kwa kuwafikishia mzigo mpaka mlangoni kwa gharama nafuu sana.

 

“Kwa wateja wa mikoani, tunawatumia mzigo mpaka mahali popote walipo. Cha kufanya ni wewe mteja kututumia oda yako ya vifaa unavyohitaji, mahali ulipo na namna ya kukufikishia, kisha mengine unatuachia sisi,” alisema Abdul Aziz.

Mbali na huduma za vifaa vya maofisini, Prince Stationery pia wanauza vifaa vya mashuleni, mapambo ya ndani, vifaa vya kisasa vya michezo ya watoto na mapambo ya sherehe kama harusi, birthday na kadhalika kwa bei poa kabisa.

 

Wasiliana nao kwa namba za simu 0774 880 082 kwa Duka la Mtaa wa Congo na 0686 942 978 kwa Duka la Mtaa wa Lindi, au unaweza kuwatembelea kwenye mitandao ya kijamii; Instagram: prince_stationery_tz, Facebook: prince stationery, Twitter: prince_ssb_tz au watumie barua pepe kwa anuani ya [email protected].

Waweza pia kuwatembelea kwenye mtandao wao kwa anuani ya www.princesecretarial.co.tz

Na Mwandishi Wetu

 

Duka Linalouza Magari ya Kifahari ya Watoto,Lazua Gumzo Kariakoo

Comments are closed.