The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Hafla ya Kuapishwa kwa Mawaziri Wapya, Dk Mwakyembe na Kabudi Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muunano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha viongozi mbalimbali wa serikali aliyowateua hivi karibuni wakiwemo Dkt. Harrison Mwakyembe na Prof. Palamagamba Kabudi aliyowateua jana.

 

Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Prof. Palamagamba Aidan Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria

Alfayo Kidato kuwa  Katibu Mkuu Ikulu

Sylvester Mabumba kuwa Balozi Comoro
Abdallah Possy kuwa Balozi Ujerumani

George Masima kuwa Balozi Israel

Stella Mgasha kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi na Mahakama

==>Haya ni mambo machache aliyoyasema Rais Magufuli Leo
1.Kuna wengine walisema Kinana leo angezungumza na waandishi, wakati nimemtuma India ambapo atakuwa kwa zaidi ya siku 10
2.Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi
3.Ukiangalia siku iliyofuata baada ya Rais wa Benki ya Dunia kuja, magazeti yote yaliandika habari nyingine tofauti-
4.Niwatake waandishi wa habari muwe wazalendo, Tanzania ikiharibika na nyie pamoja na wanaowatuma muandike wote mtaharibikiwa
5.Hata magazeti ya leo yana picha ya mtu mmoja ambaye amefanya kosa moja, utadhani kosa ni linaungwa mkono na serikali
6.Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna hiyo, kuweni makini sana
7.Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, ‘watch out’
8.Vyombo vingine haviandiki mazuri ya mtu, lakini wakipata mabaya yake ndiyo yanajaza kurasa
 
==>Tazama hii Video kumsikiliza Rais Magufuli akiongea Pamoja na walichoongea wateule wa Rais

Comments are closed.