The House of Favourite Newspapers

FUATILIA LIVE Yanayojiri Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Kenya

0

Wananchi wakiwa kwenye vituo vya uchaguzi mapema alfajiri leo.

 

IKIWA ni Agosti 8, 2017, takribani Wakenya milioni 19 wanatarajia kupiga kura kuwachagua rais, magavana wa kaunti, wabunge, maseneta, wawakilishi wa wanawake na wawakilishi wa kata.

Vituo karibu vyote vya kupigia kura vimefunguliwa rasmi tangu saa 12: 00 alfajiri, huku wapiga kura wakijitokeza vituoni kuanzia majira ya saa 9 usiku tayari kupanga foleni kwa ajili ya uchaguzi huo.

Kwa mara nyingine, Uhuru Kenyatta wa Chama cha Jubilee na Raila Odinga wa Muungano wa Upinzani (NASA), wanaonekana kuwa na ushindani mkubwa katika kinyang’anyiro hicho. Kenyatta ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta na Odinga ni mtoto wa makamu wa rais wa kwanza Jaramogi Oginga Odinga.

 

Maofisa wa Tume ya Uchaguzi wakiandaa fomu kwa ajili ya uchaguzi.

 

Waziri awahakikishia Wakenya usalama wakipiga kura

Kumekuwa na wasiwasi kuhusu hali ya usalama nchini Kenya, hasa kutokana na ushindani mkali unaoshuhudiwa kati ya wagombea urais wawili wakuu huku wananchi wao wakiwa bado wanakumbuka ghasia zilizozuka baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Aidha, hivi karibuni Meneja wa TEHAMA wa Tume ya Uchaguzi IEBC, Chris Musando aliuawa na watu wasiojulikana. Wakati huo Kaimu Waziri wa Usalama, Dkt. Fred Matiang’i amewahakikishia Wakenya kwamba usalama umeimarishwa.

 

Masanduku ya kura yakipangwa.
 
Leave A Reply