The House of Favourite Newspapers

Fundi saa awa gumzo Kampeni ya DC Kinondoni

0

1

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni (wa pili kushoto), Ally Hapi akimtazama Amani Mang’ita, mbunifu wa ujasiriamali wa kutengeneza saa.

2

DC Hapi akizungumza na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kinondoni waliohudhiria hafla hiyo (hawapo pichani).

3

Hapi akimpongeza Mang’ita kwa ubunifu wake huo.

4

Amani Mang’ita akijinadi viwanjani hapo.

5

Mjasiriamali wa kutengeneza mkaa unaotokana na takataka akimweleza Mkuu wa Wilaya changamoto mbalimbali anazokabiliana nazo.

6

Baadhi ya vikundi mbalimbali vilivyofika viwanjani hapo vikiorodhesha majina yao.

7

Hapi akiendelea kutembelea mabanda.

9

Wajasiriamali wakiendelea kutoa changamoto zao kwa DC Hapi.

FUNDI saa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Amani Mang’ita, mkazi wa Mbezi, Kimara amekuwa gumzo kubwa katika kampeni ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi ya uzinduzi wa mafunzo ya Ujasiriamali.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Agosti 20 mwaka huu  katika Viwanja vya Posta-Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo mkuu huyo alifika na kutembelea baadhi ya mabanda ya wajasiriamali.

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa mafunzo hayo kwa wakazi wa wilaya yake, Hapi alisema lengo kubwa ni kutoa elimu na mbinu mbalimbali za kuongeza wigo kwa wajasiriamali wadogo pasipo kusubiri kuajiriwa.

Alisema, waliohudhuria mafunzo hayo wahakikishe wanajiandikisha katika karatasi za majina zilizokuwepo viwanjani hapo kupitia kwa watendaji wao wa serikali za mitaa, ili waweze kupata takwimu sahihi ya wajasiriamali na wanaohitaji kuanza ili kutambuliwa ili hata kama wakikopeshwa kutoka kampuni fulani iwe rahisi kujulikana.

Aliongeza kuwa serikali haiwezi kuacha kutambua mchango wa wajasiriamari wadogo kwani wao ndiyo dira kubwa kuelekea kuongeza viwanda hapa nchini.

(Picha/Habari:  Denis Mtima/Gpl)

Leave A Reply