The House of Favourite Newspapers

THE GAME HATARINI KUKOSA MKWANJA WA ALBUM YAKE IJAYO


RAPA Mmarekani,  The Game, yupo kwenye hatari ya kukosa mirahaba yake (royalties) kwenye albam yake ijayo kwa sababu mwanamke anayedai kuwahi kunyanyaswa na rapa huyo kingono ameiomba mahakama kufanya hivyo.


Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizodakwa na mtandao wa The Blast, imearifiwa kuwa Priscilla Rainey amemuomba jaji kupata haki yake kwa kuchukua haki zote, mirahaba na kwa mapato yoyote atakayopata The Game kwa sasa hasa kupitia albam yake ijayo, Born to Rap.

 

Rainey bado anadai fidia ya ($7.2 milioni) sawa na Tsh. 16 bilioni ambayo alishinda mahakamani kwenye kesi yake ya kunyanyaswa kingono na The Game wakati wa usaili wa kipindi cha VH1 cha The Game mwaka 2015.

Comments are closed.