The House of Favourite Newspapers

Gamondi: Kila mchezaji wa Yanga atafunga

0

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuwa hawapi majukumu washambuliaji pekee kufunga ndani ya kikosi hicho bali kawapa uhuru wachezaji wote kufunga.

Ikumbukwe kwamba, kabla ya mchezo wa jana dhidi ya Coastal Union uliotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Yanga ilikuwa ni namba moja kwa kufunga mabao mengi.

Ni mabao 25 yalikuwa kibindoni baada ya kucheza mechi 8, huku ukuta wake ukiruhusu mabao matano ndani ya dakika 720.

Mtupiaji wa bao la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga ni Dickson Job ambaye ni beki, alifunga kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar, dhidi ya KMC.

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema kuwa wachezaji wote wana kazi ya kutafuta matokeo uwanjani, hivyo ni lazima watumie nafasi ambazo wanazipata bila kujali anacheza nafasi gani.

“Unaona kwenye mabao mengi ambayo tunafunga washambuliaji wetu hawajafunga mabao mengi. Ipo hivyo kulingana na namna ambavyo wachezaji wanashirikiana kwenye kutimiza majukumu.

“Viungo wanafunga mabao kwenye mechi wanazocheza, mabeki nao wanafunga hivyo kila mchezaji kwenyetimu ana uhuru wa kufunga ili kuipa timu matokeo kikubwa ni pointi tatu muhimu na kucheza vizuri,” alisema Gamondi.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply