The House of Favourite Newspapers

Toyota Spacio Yapata Ajali Sinza, Dar

Muonekano wa gari baada ya ajali.

GARI dogo aina ya Toyota Spacio leo jioni limepata ajali baada ya kuacha barabara na kuingia mtaroni eneo la Sinza-Mori jijini Dar es Salaam na kuharibika kwa kiasi kikubwa.   Hata hivyo, hakuna mtu aliyeumia licha ya uharibifu wa gari hilo na kibanda cha biashara kilichokumbwa na gari hilo.

Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la tukio.

Mashuhuda wa ajali hiyo walisema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa gari hilo ambapo ghafla alikutana na mwendesha bodaboda na wanafunzi watatu mbele yake,  hivyo katika kuwakwepa alijikuta gari likimshinda na kupoteza mwelekeo kisha kuingia mtaroni na kugeukia lilikokuwa likitoka.

Juhudi za kulitoa gari mahali pa ajali zikifanyika.

Comments are closed.