The House of Favourite Newspapers

Baada ya Kikao Kizito, Hatimaye Muna Akubali Kupeleka Msiba kwa Peter

KUFUATIA sintofahamu kuhusu baba halisi wa mtoto wa mwigizaji wa Bongo Movie, Muna  na wapi msiba upelekwe, muigizaji wa Bongo Movie ambaye pia ni kiongozi wa tasnia hiyo aliyeshiriki kupata ufumbuzi wa suala hilo, Steve Mengere ‘Nyerere’, hatimaye (Muna) mama wa mtoto marehemu Patrick, amekubali msiba upelekwe kwa baba wa marehemu ambaye ni  Peter Zacharia maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ‘Nyerere’ amesema amezungumza na Muna na kufikia maridhio hayo kwa pande zote za wazazi wa mtoto huyo.

Hayo yamejiri ikiwa ni baada ya kikao cha muda mrefu kati ndugu wa familia ya Muna na Peter kumsihi Muna ili waungane na baba wa mtoto huyo kufanikisha shughuli ya kumsitiri pamoja Patrick.

Mbali na Steve Nyerere, wasanii wengine waliokuwepo ni Shamsa Ford, huku Wema na mama yake wao walifika jana na kusema wasingeweza kwenda Mbezi kwa Muna kwani wanamfahamu Peter ndiye baba wa mtoto huyo.

VIDEO: BABA HALISI WA PATRICK AFUNGUKA MAZITO, KIFO CHA MWANAYE

 

Comments are closed.