The House of Favourite Newspapers

Gari la Salamba Lapata Ajali

 

MSHAMBULIAJI wa Simba, Adam Salamba aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Lipuli FC ya mkoani Iringa amekumbana na balaa kubwa juzi Jumamosi baada ya gari yake kupata ajali.

Gari hilo ni lile ambalo alipewa hivi karibuni na uongozi wa Simba mara baada ya kuingia mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo.

 

Ajali hiyo ilitokea juzi jioni eneo la Vigwaza mkoani Pwani wakati gari hilo lilopokuwa likitolewa mkoani Mwanza na dreva kuletwa Dar ambapo Salamba anaishi sasa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Salamba alisema kuwa baada ya kupewa gari hilo alienda nalo Mwanza na kuliacha huko lakini hivi karibuni alimwagaza dreva mmoja wa Simba akamletee na ndipo likapata ajali.

 

“Ni kweli kabisa gari yangu imepata ajali maeneo ya Vigwaza baada ya kugongwa kwa nyuma na lori kisha nalo likaenda kuigonga gari nyingine iliyokuwa mbele.

Ukweli ni kwamba limeharibika sana. Hata hivyo, hakuna mtu aliyeumia katika ajali hiyo jambo ambalo ni la kumshukuru Mungu ,” alisema Salamba wakati alipokuwa njiani akielekea eneo ilipotokea ajali hiyo akiwa ameambatana na kocha wake wa zamani Selemani Matola.

 Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam.

Comments are closed.