The House of Favourite Newspapers

Gari la STK lazua Kizaazaa Gereji Moro

0

stk

MOROGORO: Katika hali isiyokuwa ya kawaida, gari moja lenye namba za usajili za aina mbili ikiwemo ya serikali ya STK limeleta kizaazaa kwenye gereji moja mjini Morogoro, Amani limejuzwa.

Kwa mujibu wa chanzo, gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser VX liliingia kwenye gereji hiyo iliyopo Mji Mpya Jengo la Sido huku  baadhi ya mafundi wakishangaa kwa vile, wanajua agizo la serikali kwa sasa ni magari yote ya serikali kwenda kwenye gereji za serikali.

“Jamani hapa Jengo la Sido kwenye gereji binafsi, kuna gari limeingia lina namba za usajili aina mbili, namba za STK na za binafsi. Lakini sasa yote tisa cha ajabu ni kwamba, lilipoingia lina namba binafsi, lakini kwenye vioo bado lina namba za serikali.

“Hilo moja, pili, baada ya kuingia likanyofolewa pleti za binafsi likabaki halina pleti,” kilisema chanzo chetu.

Amani lilifunga safari mpaka kwenye gereji hiyo lakini dereva wake alipomwona paparazi wetu aliondoka. Amani lilizungumza na fundi mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina lake akisema:

“Mimi ninavyojua hili gari lilikuwa la serikali lakini likauzwa. Ilibidi namba za kwenye vioo ziondolewe. Hao wanaosema limeingia kama gari la serikali hawajajua tu ndiyo maana wengi wameshangaa wakiamini dereva amekiuka agizo la serikali,” alisema fundi hyo huyo.

Leave A Reply