The House of Favourite Newspapers

Gari Linalopaa Lakamilika

0

DUNIA inakwenda kasi sana na kama huamini, sikia hii; gari-ndege ni gari lenye uwezo wa kupaa angani ambalo linakaribia kuzinduliwa baada ya kupiga hatua muhimu ya kukamilisha dakika 35 angani, gari hilo linaelezwa kuwa, lina injini ya gari la BMW na linatumia mafuta ya petroli.

 

Majaribio ya gari hilo yamefanywa katika Viwanja ya Ndege vya Kimatifa huko Nitra na Bratislava nchini Slovakia, siku ya Jumatatu ya Juni 28, mwaka huu.

 

Mvumbuzi wa gari hilo, Stefan Klein anasema kuwa, gari hilo lina uwezo wa kupaa angani kwa zaidi ya kilomita 1,000 na urefu wa juu wa futi 8,200.

 

Klein anasema kuwa, gari hilo linachukua dakika mbili na sekunde 15 kubadilika kutoka kuwa gari hadi ndege, Likiwa angani, gari hilo lilikuwa na kasi ya kilomita 170 kwa saa.

 

Mvumbizi wa gari hilo pia anasema kuwa, lina uwezo wa kuwabeba watu wawili wenye uzito wa kilo 200 na linahitaji barabara ya ndege, ingawa likilinganishwa na ndege zisizo na rubani linaweza kupaa wima.

 

Uvumbuzi huu unakuja wakati kuna matarajio mengi kuhusu ugunduzi wa magari ya kupaa angani ambayo yamekuwa yakisalia kama utabiri.

Stori: Sifael Paul

Leave A Reply