The House of Favourite Newspapers

GAZETI SPOTI XTRA ALHAMISI LAZIDI KUTIKISA

KAMA kawaida,  leo tena timu ya wafanyakazi wa Global Publishers, wakiwemo wahariri wa magazeti ya kampuni hiyo, wameingia  mitaani kuendelea kulinadi gazeti la michezo la Spoti Xtra ambalo ni jipya  lililoingia mitaani Alhamisi ya wiki iliyopita kwa bei ileile ya shilingi 500.

Akizungumzia ujio huo wa gazeti la Spoti Xtra kila Alhamisi,  Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Pau,  amesema kwa wapenzi wa habari za michezo  gazeti hilo ndiyo sehemu sahihi ya kumaliza kiu yao ya habari za michezo, hivyo  walinunue gazeti tena kwa bei ileile ya  sh. 500 tu.

Nao baadhi ya wasomaji wa gazeti la Spoti Xtra ambao walichangamkia kulinunua maeneo ya stendi ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo,  wamelipongeza kwa mwonekano mzuri na kwa namna ambavyo limesheheni habari za michezo na hivyo wakasisitiza juu ya kulinadi kwa wingi mtaani ili kila mpenda soka kuweza kuliata.

“Global mmetusaidia  kuliingiza gazeti hilo siku ya Alhamisi kwani tumekuwa tukikosa habari za michezo kwa siku hiyo, hivyo endeleeni kulisambaza kila kono ya nchi ili wadau wapate habari za michezo,” alisema  mmoja wa madereva wa stendi hiyo  aliyejitambulisha kwa jina la  Abubakar Juma.

Matukio katika Picha:

Comments are closed.