The House of Favourite Newspapers

Generation Africa Yatangaza Washindi Wawili Tuzo Ya USD 100,000

0
Daniella Kwayu, CEO Phema Agri Tanzania

Washindi hao walijinyakulia kitita hicho katika shindano la GoGettaz Agripreneur kwa mwaka 2020, pamoja na tuzo heshima za chakula Afrika katika kongamano la Afrika Green Revolution Forum Virtual Summit nchini.

Kongamano hilo lililofanyika Septemba 11 lenye lengo la tuzo hii ni kuwaibua na kuwahamasisha vijana barani afrika kukamata fursa katika mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo cha chakula wenye thamani ya  $1Tn barani ndani ya miongo michache ijayo.

Wakizungumza wakati wa kongamano hilo, Moses Katala muasisi mwenza na CEO wa magofarn Limited Rwanda na Daniel Kwayu muasisi mwenza na CEO wa Phema Agri Tanzania ni kwamba kila mshindi atapokea dola 50,000 kwa ajili yakusaidia na kupanua uendeshaji wa biashara yao ya kilimo.

Moses Katala CEO Mago Farm Ltd Tanzania.

Kwayu, alisema wajasiriamali wengine wanne vilevile walitajwa kupokea tuzo ya $2,500 ya athari (Impact Award) Elizabeth Gikebe, muasisi na CEO wa Mhogo Foods (Kenya), Millicent Agidipo, muasisi mwenza na Meneja Uzalishaji wa Achiever Foods (Ghana), Dysmus Kisulu, Muasisi mwenza na CEO wa Solar Freeze (Kenya) na Paul Matovu,muasisi na CEO wa Vertical Farm and Micro-Gardening (Uganda).

“Wajasiriamali hawa walichaguliwa na majaji kwa kuonyesha athari chanya katika mazingira au kwa jamii wanazotokana na biashara zao, kila mmoja akiwa anajitahidi kufikia malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu na kunufaisha jamii zao.

“Wajasiriamali wote 12 walioingia fainali na  watapata ushauri, kuunganishwa na programu pamoja na kupata miongozo ya kuendelea na safari yao ya ujasiriamali,”alisema.

Leave A Reply