The House of Favourite Newspapers

Nameless Awaonya Warembo: Msidanganywe na ‘Six Pack’

0

MSANII wa muziki nchini Kenya, David Mathenge almaarufu Nameless, kwa muda amekuwa akitoa maoni yake kwenye mitandao ya kijamii, huku akiwashauri mashabiki wake.

 

Kama baba wa wasichana ambao wamo katika umri wa ujana wao hajaacha wasichana na wanawake kudanganywa na wanaume ambao hawamo tayari kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na wao.

 

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya Instagram, Nameless aliposti video akicheza akiwa katika chumba chake cha kulala na kwa mara ya kwanza alionyesha kifua chake.

 

Baada ya kupakia video hiyo aliandika ujumbe akiwaonya wasichana dhidi ya kupenda wanaume wenye kifua kikubwa wakidhani  kwamba wana pesa.

 

“Wanaume wa one pack mpo? Wasichana msidanganywe na wanaume wa six pack, hawakuagi na pesa akiba yao yote huenda kwa gym na chakula. Jipatie mwanamume wa one pack,” aliandika Nameless.

Leave A Reply