The House of Favourite Newspapers

Gesi Yazuia Wafanyabiashara Kuendelea na Shughuli Zao KariaKoo

0

KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John Masunga amesema kutokana na ukubwa wa eneo lililoungua bado kutaendelea kuwa na gesi ambayo haifai, hivyo wafanyabiashara hawataweza kufanya  shughuli zao hadi pale watakapopewa taarifa rasmi.

 

Masunga ametoa kauli hiyo leo Jumapili Julai 11, alipotembelea soko hilo kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kuangalia eneo lililoshika moto. amesema taarifa za moto zilipokewa katika Kituo cha Zimamoto Ilala saa 2:40 usiku.

 

Masunga amesema hadi kufikia kesho haitawezekana wafanyabiashara kuendelea na shuguli zao kutokana na uwepo wa gesi ambayo haifai.

 

“Nimefika hapa kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kuangalia eneo lililoshika moto, kwa kweli nimeshuhudia moto ulikuwa ni mkubwa sana na kazi ya kuzima moto huo ilifanyika vizuri kwa kuwa Jeshi la Zimamoto na Ukoaji lilikuwa limejiandaa vilivyo.

 

“Tulipata changamoto mbili wakati wa kuzima moto, kwanza hapa katika Soko la Kariakoo sehemu za kuchukulia maji hazitoi maji, hivyo ilitubidi twende mbali kwa ajili ya huduma hiyo na tatizo la pili ni watu kuzingira eneo la tukio hali iliyosababisha magari yetu kushindwa kuingia na kutoka kwa urahisi,” amsema Masunga.

 

 

Leave A Reply