The House of Favourite Newspapers

Gethsemane Group Kinondoni GGK (GGK) Waja Na Video Ya Bwana Wastahili

0

Dar es Salaam, 18 Machi 2024: Waimbaji maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video ya wimbo wao mpya unaoitwa Bwana Wastahili.

Video ya wimbo huo imeachiwa leo Machi 18,2024 saa mbili usiku na imerekodiwa katika Studio ya Flying Wave na kuongozwa na Director maarufu ajulikanae kama Director Joowzey.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya video hiyo kuachiwa hewani (kuzinduliwa) Mwenyekiti wa Gethsemane Group Kinondoni (GGK) Geoffrey Joseph amesema ni furaha kwao kuja na video ya wimbo huo ambayo imebeba ujumbe wa kumuabudu na kumtukuza Mungu.

“Ujumbe mkubwa kwenye wimbo huu ni kwamba Mungu pekee ndie anastahili kuabudiwa na yeye ndiye anatosha kwa kila kitu hasa kipindi hiki ambacho baadhi ya madhehebu wapo kwenye mfungo hivyo tunaamini wimbo huu ni ibada na utawasogeza karibu zaidi na Mungu,”amesema Joseph.

Aidha ametoa neno kwa wasikilizaji na watazamaji wa video ya wimbo huo kutambua hakuna yoyote anayestahili kuabudiwa zaidi ya Mungu pekee.

Leave A Reply