The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Andaeni Mpango Wa Ufadhili Wataalamu Wa Kiswahili

0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia, iandae mpango maalum wa ufadhili wa wataalam wa lugha ya Kiswahili kwenye ngazi ya shahada ya uzamivu ili kukidhi mahitaji sambamba na kuimarisha mafunzo ya lugha kwa ajili ya kuzalisha wataalam na wakalimani wa kiswahili wenye viwango vya kimataifa.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo Jumatatu, Machi 18, 2024 wakati alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Kongamano la Nne la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika katika Hoteli ya Eden Highlands jijini Mbeya.

Amesema Serikali imeendelea kuchukua hatua kadhaa ili kukibidhaisha Kiswahili na moja ya hatua hizo ni kuandaa Mkakati wa Taifa wa kubidhaisha Kiswahili ambao una lengo la kuifanya lugha hiyo kuwa bidhaa kwa kutoa fursa za kujikwamua kiuchumi kwa rasilimaliwatu wanaojihusisha nayo pamoja na watoa huduma za kiswahili.

“NA WEWE BOSI WAO -HAIWEZEKANI -UTAKOMESHWA na MUNGU SIKU UKIFA” – #TBT MAGUFULI GEREZA la UKONGA..

Leave A Reply