The House of Favourite Newspapers

Ghorofa Laporomoka, Watu 10 Wafariki Dunia

0

Idadi ya watu waliofariki baada ya kuporomoka kwa hoteli moja iliyokuwa ikitumiwa kuwaweka watu chini ya karantini kutokana na virusi vya corona katika mji wa Quanzhou nchini China, imefikia watu 10.

 

Mamlaka nchini humo zimesema watu wengine 28 bado wamekwama kutokana na ajali hiyo. Awali zaidi ya watu 70 waliaminika kukwama katika jengo hilo la ghorofa saba lililoporomoka jana jioni.

 

Wakati wa mkutano na wanahabari uliondaliwa na serikali katika eneo la Quanzhou jana, maafisa wa serikali, wamesema kuwa kikosi cha uokoaji cha zaidi ya watu elfu moja ikiwa ni pamoja na maafisa wa zima moto, vikosi vya polisi pamoja na wahisani wengine, walifika katika eneo hilo juzi usiku huku watu 43 wakiokolewa na 36 kati yao kupelekwa hospitalini.

 

Shirika la habari nchini humo Xinhua, limeripoti kuwa ghorofa ya kwanza ya jengo hilo ilikuwa chini ya ukarabati wakati wa tukio hilo.

 

Leave A Reply