The House of Favourite Newspapers

Gigy aapa kumkomesha Diva!

0

GIGY (2)Gift Stanford ‘Gigy Money’

Stori: Mayasa Mariwata, Wikienda

DAR ES SALAAM: MWANADADA asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ ambaye ni Mtangazaji wa Radio Choice FM ameapa kumkomesha mtangazaji mwenzake wa Clouds FM, Loveness Malinzi ‘Diva’ kutokana na bifu zito linaloendelea kati yao akisisitiza kumkwapulia bwana’ke.

diva1Loveness Malinzi ‘Diva’

Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na mashosti hao, siku chache zilizopita walishikana ushosti sasa hivi wapo kwenye bifu zito hadi kufikia hatua ya kupigana vijembe mitandaoni kwa madai kuwa Diva anajitapa kumtafutia Gigy kazi ndani ya Choice FM huku video queen huyo akipingana na kauli hiyo.

Kutokana na ishu hiyo, Diva alipotafutwa alijibu kwa kifupi kuwa hamjui Gigy na hataki kuulizwa ishu hiyo. Kwa upande wake Gigy alikiri kuwa kwenye bifu zito na mwanadada huyo akisema kuwa, akiendelea kumchokonoa, lazima ampindue kwa mwandani wake.

Leave A Reply