The House of Favourite Newspapers

Kanye atikisa mitandao!

0

kanye-west-famous-music-video-source-tidal-added-black-cover-671x377 NEW YORK, Marekani

STAA wa Hip Hop kutoka Marekani, Kanye West hivi karibuni alitikisa mitandao mbalimbali baada ya picha zake kuvuja akiwa utupu na mastaa feki wengi.

Kwa mujibu wa Jarida la Vanity Fair la Marekani, picha hizo zinazosambaa zinawaonesha utupu mastaa feki wakiwa kitandani kwa pamoja ambao ni Ray J, Caitlyn Jenner, Billy Cosby, Amber Rose, Kim Kardashian, Tylor Swift, Chris Brown, Rihanna, Donald Trump, Anna Wintour na George W. Bush.

Famous“Kanye ana mpango wa kuja na video ya Wimbo wa Famous ambao utakuwa ni wa saba kuachiwa katika albamu yake ya The Life of Pablo. Video hiyo inatarajiwa kuvunja rekodi ya dunia kwa kuwaanika mastaa (feki) wa dunia wakiwa utupu kitandani na itaanza kupatikana kupitia mtandao wa muziki wa Tidal,” ilisema sehemu ya jarida hilo.

Katika picha hizo zinamuonesha Kanye West akiwa mtupu kitandani akiangaliana na mkewe, Kim Kardashian huku nyuma akizungukwa na mastaa wengine feki wengi.

Leave A Reply