The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 02: Hatimaye KAGAME Apokea Kijiti cha Mwenyekiti EAC – VIDEO

Rais wa Rwanda Paul Kagame amepokea kijiti kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa afrika Mashariki kutoka kwa rais wa Uganda Yoeli Kaguta Museven huku nchi yake ikiwa katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na nchi ya Burundi. Rais Paul Kagame akiwa katika mkutano wa 20 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki mjini Arusha alikabidhiwa uongozi huo na raisi wa Uganda Yoel Museven baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka miwili.

Nchi ya Rwanda imeingia katika mgogoro wa Kisiasa na Burundi baada ya Utawala wa Bujumbura kuituhumu serikali ya Rwanda kwa kuvisaidia vikundi vya waasi na wapinzani wanaopinga muhula wa tatu wa utawala wa Rais Pierre Nkurunziza.

Mvutano huu uliipelekea Bujumbura kuulalamikia uongozi wa EAC kuwa unafumbia macho tuhuma hizo hivyo kuamua kususia mara kadhaa vikao vya umoja huo.

Hata hivyo kamati ya usuluhishi wa mgogoro huo wa Rwanda na Burundi chini ya aliyekuwa mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya Tatu Benjamini mkapa katika kikao chake cha ndani imetoa taarifa ya kuendelea kwa usuluhishi wa mgogoro huo.

Comments are closed.