The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 16: WAZIRI MKUU ATINGA KIGOMA ZIARA YA SIKU NNE – VIDEO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo feb 16, amewasili mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku nne, ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga wakati alipowasili katika Uwanja wa Ndege mkoani humo.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu, Majaliwa ameambata na mkewe bi Mary Majaliwa,na mara baada ya kuwasili uwanjani hapo amepata nafasi ya kuwasalimia wananchi wa mkoa wa kigoma waliojitokeza kumlaki.

Lengo la ziara hiyo ni kuweka mkazo na msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na kukagua vitalu, mashamba kwa lengo la kuboresha zao hilo la biashara nchini.

Akiwa mkoani Kigoma, Waziri Mkuu atatembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo wilayani kibondo na kuzungumza na wakimbizi sambamba na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya chama cha mapinduzi CCM, na utekelezaji wa miradi pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo atakayotembelea.

Comments are closed.