The House of Favourite Newspapers

Global Habari Feb 23: Mchango Wa Sekta Ya Madini Kwenye Pato La Taifa

0

Sekta ya madini imetajwa kuwa ya pili katika kuchangia kwenye pato la taifa kwa mwaka 2019/20 huku ukusanyaji wa mapato ukiongezeka na kufikia asilimia 51.5 kwenye nusu ya kwanza ya malengo ya mwaka ya ukusanyaji mapato wa sekta hiyo.

 

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Tanzania KASIM MAJALIWA wakati akihitimisha mkutano wa siku mbili wa kimataifa kuhusu uwekezaji katika sekta ya madini nchini kwa mwaka 2020 uliobeba kauli mbiu ya “Uwekezaji na Ushiriki katika sekta ya madini” ambapo pamoja na mambo mengi kumefanyika uzinduzi wa Hati za uhalisia kwa madini ya aina tatu (yaani three T) ikiwa ni makubaliano ya ushirika kwenye nchi za maziwa makuu kwa lengo la kunufaisha wanachi.

Leave A Reply