The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI JAN 19: Maamuzi ya Waziri Mkuu Baada ya Kukagua Ujenzi wa Hospital

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na kusema uamuzi huo ni utekelezaji wa agizo la serikali wa kuwa na kituo cha afya kila kijiji.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani chamwino ,Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya maeneo mengine kutokana na manufaa yake kwa umma.

Comments are closed.