The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI MACHI 06: Rais MAGUFULI Alivyoshiriki Ibada ya Majivu Leo – VIDEO

Rais Dr John Magufuli leo ameungana na waumini wa madhehebu ya kikatoliki duniani katika ibada maalumu ya kupaka majivu ikiwa ni mwanzo wa kipindi cha mfungo wa kwaresma.

Ikiwa ni Jumatano ya Majivu March 6, mwaka huu Rais Magufuli akiongozana na Mkewe mama Janeth Magufuli walifika katika kanisa la mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kushiriki Ibada hiyo Muhimu kwa Wakristo.

Baada ya Ibada hiyo Rais Magufuli alipata nafasi ya kushikana mkono na waumini wenzake huku akiwatakia mfungo mwema wa kwarezima kwa kumkumbuka Yesu Kristo juu ya mateso aliyoyapata wakati wa kumkomboa mwanadamu.

Leo March 6, ni Jumatano ya majivu ambapo wakristo wameanza mfungo wa Kwarezima na Wakristo hutumia Kipindi hiki Kusikiliza, kutafakari na kuishi Neno la Mungu katika uhalisia wa maisha yao.

Comments are closed.