The House of Favourite Newspapers

Global Habari Nov 8: JPM Awataka Viongozi Afrika Wasitegemee Misaada – Video

Rais Dkt. John Magufuli amewataka viongozi Barani Afrika kujenga mfumo wa kujitegemea kiuchumi ili kuondokana na fikra tegemezi katika kujikwamua kiuchumi.

 

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kwa nchi za Afrika pamoja na Nchi za Nordic ambao umefanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na viongozi wastaafu akiwemo Rais Mtaafu Awamu ya Nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Comments are closed.