The House of Favourite Newspapers

Saleh Ally Awa Mhariri Mtendaji Global Publishers

mtendaji-11

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia) akiwa na Mhariri Mtendaji mpya Saleh Ally (wa pili kutoka kushoto), Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho (kushoto) na  Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumatano, Ojuku Abraham (wa pili kutoka kulia).

mtendaji-3

Saleh Ally (katikati) akiwa na mhariri wa Championi Jumatano, Philip Nkini (kushoto),  Mhariri wa Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula (wa pili kushoto) Mhariri wa Championi Ijumaa, John Joseph (kulia) na Ofisa Masoko, David Mwaipaja (wa pili kutoka kulia).

mtendaji-4

 Kutoka kushoto  ni Philip Nkini, Ezekiel Kitula, Eric Shigongo, David Mwaipaja, John Joseph, Musa Mateja, Said Ally na aliyechuchumaa ni Omary Mdose wakiwa na Saleh Ally.

mtendaji-1

Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Oscar Ndauka (katikati) akiongea jambo na Saleh Ally na wafanyakazi wengine.

mtendaji-8mtendaji-12

mtendaji-8 mtendaji-2 mtendaji-4 mtendaji-6 mtendaji-7

mtendaji-14

Wafanyakazi wa Global wakiwa na Saleh Ally.

Aliyekuwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally ameteuliwa kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd kuanzia Ijumaa iliyopita.

Akizungumza leo na wafanyakazi wa Global, Saleh amesema amepokea uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na wafanyakazi wote katika kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo la kampuni.

“Nimepokea kwa mikono mwili uteuzi huu, lakini najua kazi hii ili nifanikiwe ni lazima nishirikiane na nyinyi. Nilikuwa Mhariri Kiongozi wa magazeti ya Championi lakini sasa ni kiongozi wa magazeti yote katika kampuni yetu, nawaahidi nitafanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu na kila mmoja,” alisema.

Naye Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema kuteuliwa kwa Saleh ni uthibitisho kwamba ni kiongozi mzuri mwenye uwezo wa kuongoza katika tasnia ya habari, hivyo alimpongeza kwa kupewa wadhifa huo. Saleh Ally amechukua nafasi iliyoachwa na Richard Manyotta ambaye sasa hayupo katika kampuni hiyo.

Licha ya kufanya kazi katika Kampuni ya Global, Saleh Ally amewahi kufanya kazi ya habari katika makampuni mbalimbali kama Mwananchi na Habari Corporation.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.