The House of Favourite Newspapers

Global Publishers yawapongeza Lulu, Richie kwa tuzo

0

2
Lulu akipongezwa na waziri mkuu Majaliwa.

Mwandishi wetu, amani

UONGOZI na wafanyakazi wa Global Publishers wanaochapisha magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Championi, Risasi Jumatano, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi wanawapongeza wasanii wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Single Mtambalike ‘Richie’ kwa kutwaa Tuzo za Africa Magic Viewers Choice 2016 zilizofanyika Machi 6, mwaka huu jijini Lagos, nchini Nigeria.

Richie alipata tuzo kupitia filamu yake ya Kitendawili, akishinda kipengele cha filamu ya Kiswahili (Best Indigenous Language Movie/ TV Series-Swahili) huku Lulu akishinda kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu kipengele cha Filamu Bora Afrika Mashariki (Best Movie- Eastern Africa).
Ushindi wa Lulu na Richie umewafanya Watanzania kutembea kifua mbele kila wanakokwenda nje ya nchi kutokana na kumbukumbu za baadhi ya Watanzania wengine waliowahi kutwaa tuzo nje ambao ni Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na msakata kabumbu Mbwana Samatta.

Kampuni ya Global inawataka wasanii wengine wa filamu na fani nyingine nchini kutorudi nyuma wakiamini hawawezi kwani kwa sasa, Mtanzania kutwaa tuzo kimataifa siyo jambo gumu kama zamani. Hongera sana Lulu, hongera sana Richie.
Global inawataka Watanzania wote kuwaunga mkono wasanii wetu kwa kununua kazi zao halisi (orijino) ili kuinua juu tasnia husika na kutoa ajira kwa wengi.

3Richie akipongezwa na waziri mkuu.

Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

Kadja Nito
adaiwa kuchumbiwaMayasa Mariwata
MWANADADA anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ anadaiwa kuchumbiwa na kigogo mmoja (jina kapuni) hali inayomfanya kukaa kimya kimuziki.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilicho karibu na msanii huyo, bi’shosti huyo aliyekuwa akibamba na Wimbo wa Sina Maringo amekuwa akionekana viwanja mbalimbali akijiachia na kigogo huyo.

“Sasa hivi mambo yake yamemnyokea, ndiyo maana siku chache zilizopita alionekana akila bata Sauzi, japo haonekani akipiga dili zozote zinazohusiana na kazi zake za kimuziki,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kunasa madai hayo, Showbiz Xtra ilimvutia waya Kadja kujua kama kuna ukweli ambapo alifunguka;
“Hilo la kuchumbiwa siyo kweli jamani, ni kweli sionekani kupata dili za shoo hivi karibuni lakini siyo kwamba nimefichwa na mtu, hapana! Niwaambie tu mashabiki wangu, soon mtaona mambo makubwa kutoka kwangu sababu Sauz nilienda kikazi siyo kuuza sura kama wengi wanavyodhani.”

Leave A Reply