The House of Favourite Newspapers

Global Walivyoshiriki Msiba wa Mama wa Mhariri Stambuli

0
Elvan Stambuli akiwa mbele ya waombolezaji waliobeba mwili wa marehemu wakati ukiingia nyumbani Kisemvule Pwani tayari kwa ibada ya kumuaga na kumsafirisha kuelekea Masasi mkoani Mtwara kwa mazishi.

Ilikuwa ni siku ya huzuni sana juzi Jumatano ambapo wafanyakazi wa Makampuni ya Global Group waliungana na na familia na waombolezaji katika ibada ya kuuaaga mwili wa mama mzazi wa mfanyakazi mwenzao, Mhariri wa Magazeti ya Global Publishers, Elvan Stambuli, Bi. Mary Stambuli.

Majonzi mwili ukiwasili.

Mazishi hayo yalifanyika Kisemvule mkoani Pwani na mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda nyumbani kwao, Masasi mkoani Mtwara kwa ajili ya mazishi ambayo yalifanyika jana Alhamisi.

Wafanyakazi wa Global na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu.
Mkurugenzi wa Global, Lydia Bukumbi (kulia) na wafanyakazi wenzake, Imelda Mtema (kushoto) na Naila wakiwa na waombolezaji wengine msibani hapo.
Wafanyakazi wa Global, kutoka kushoto, Richard Manyota, Richard Bukos, Erick Evarist na Imelda mtema wakiwa kwenye ibada ya kumuaga marehemu muda mfupi kabla ya kusafirishwa.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL   

Leave A Reply