The House of Favourite Newspapers

Global Yamwaga Tecno CX kwa Mashabiki wa Instagram, Bado Hujachelewa!

KAMPUNI ya Global Publishers kupitia akaunti yake ya Instagram @globalpublishers, kama kawaida yake kuwajali mashabiki wake umekuja na zawadi kabambe ya kufungua mwaka, ambapo kesho Ijumaa zawadi ya simu mpya aina ya Tecno Camon X (CX) itatolewa kwa mshindi wa shindano lililoanza Jumapili na linaeendelea kwenye akaunti hiyo.

Akizungumzia shindano hilo, Mratibu wa Shindano, Edwin Lindege ambaye pia ni Meneja wa Iadara ya Tehama ya kampuni hiyo amesema shindano linaendelea vizuri na watu wanajitokeza kwa wingi kushiriki.

“Kama kawaida yyetu, @GlobalPublishers, huwa hatupepesi macho, tunaendela kuwaporomoshea mizigo ya zawadi bureee kila kukicha kwa mashabiki wetu, katika Msimuu huu wa Sikukuu ya Mwaka Mpya 2018, tunakupa nafasi za Kujishindia zawadi ya Smartphone aina Tecno Camon X (CX).

“Mshiriki anatakiwa ku-Follow akaunti yetu ya Instagram @GlobalPublishers kama bado hujafanya hivyo na kisha Like, share piga picha simu yako ikionnyesha umetu-follow na ututumie kupitia WhatsApp 0753 715 779 au DM. Acha komenti yako kwa kujibu swali lililopo hapo juu, kuonyesha umeshiriki.

“Tag rafiki yako yeyote, (unaweza kuwatagi marafiki wengi zaidi kadri uwezavyo).
Malizia kwa kuandika Hash Tag ya; #InstallGlobalPublishersApp (hii itakuongezea nafasi ya kushinda zawadi zaidi ya moja). jambo lingine kukuwezesha kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda, install Application ya Global Publishers, piga picha simu yako ikionnyesha App hiyo na ututumie kupitia namba hiyo hiyo au DM.

“Droo ya kumpata mshindi itachezeshwa kesho Ijumaa, Januari 5, saa 10:00 jioni na mshindi atatangazwa kesho hiyo hiyo, hujachelewa unaweza kushinda simu hiyo, endelea kufuatilia mitandao ya Global Publishers ya instagram, Facebook, twitter, website (www.globalpublishers.co.tz), YouTube (Global TV Online) na application ya Global Publishers ” alisema Lindege.

 

FUATA MAELEKEZO HAYA UJINYAKULIE SMARTPHONE MPYA

Comments are closed.