GLOBAL YATUNUKIWA TUZO NA DSJ
Chuo cha Uandishi wa habari cha Dar es Salaam (DSJ) jana Ijumaa Dec 21 kilifanya Mahafali yake ya 23 na kutuo tuzo mbalimbali kwa wadau wake, wakiwemo Global Publishers kwa kutambua mchango wake katika kuwapa nafasi wanafunzi wake kufanya mafunzo yao kwa vitendo.
Katika hotuba yake, Mkuu wa Chuo hicho Joachim Rupepo, mbele ya wahitimu 156 na na mgeni rasmi, aliishukuru Kampuni ya Global Publishers kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kwa vitendo pamoja na kuwapa ajira wanafunzi wengi wanaotoka chuoni bila vikwazo, ukilinganisha na baadhi ya makampuni mengine ambayo hutoa nafasi hizo kwa malipo.
Wahitimu wa kozi ya utangazaji wakionesha umahiri wao wa kutangaza.
(PICHA / HABARI: RICHARD BUKOS)
Comments are closed.