The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrityUpdates: Rapa Wa South Africa AKA na Mpenzi Wake Bonang Waachana!

Rapa kutoka South Africa AKA ametangza kuachana na mpenzi wake ambaye pia ni mtangazaji maarufu nchini South Africa, Bonang Matheba masaa machache yaliyopita.

Kupitia page yake ya Twitter, rapper huyo ameamua kuanika hisia zake kuhusu kuvunjika kwa uhusiano huo akisisitiza kuwa walijaribu kudumisha upendo lakini imeshindikana. Licha ya hivyo hii siyo mara ya kwanza kwa wawili hao kutangaza kuachana alafu badaae kurudiana, huenda mastaa hao wakarudiana tena siku chache zijazo.

Kuchochea uvumi wa taarifa hizo kwenye mtandao huo wa kijamii, rappa huyo ametoa ushauri wa bure kwa wanaume wenzake kwa kuwashauri wasije wakampenda mwanamke kushinda jinsi ambavyo mwanamke atawapenda wao.

Hizi hapa chini ni tweets zake zote ambazo nimezitafsiri kwa ajili yako mdau…

>> “Hata upumbavu una mwisho wake…”<<

>> “Nasikitika kuwaambia kuwa mimi na Bonang tumeachana. Tulijaribu jamani!”<<

>> “Washkaji, msije mkampenda mwanamke zaidi ya akupendavyo wewe..”<<

Usisahau kusubscribe kwenye YouTube channel yetu Global TV Online ili uweze kupata updates, taarifa na matukio yote on time, pia kaa karibu na sisi kwenye Instagram kwa ku-tufollow kupitia @globalpublishers.

Comments are closed.