The House of Favourite Newspapers

Gomes Ahamishia Hasira Kwa Yanga

0

LICHA ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa Didier Gomes, bado anawawaza watani wake Yanga akiahidi kulipa kisasi.

 

Mfaransa huyo hivi sasa yupo katika mawindo makubwa ya kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Simba. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika huko mkoani Kigoma utakaozikutanisha timu hizo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa ubingwa wao wa ligi waliouchukua hautakuwa mtamu kama wasipowafunga Yanga kwa ajili ya kulipa kisasi.

Gomes alisema kuwa, tayari amefanya kikao na wachezaji na kuwasisitiza umuhimu wa mchezo huo wa fainali aliopanga kushinda ili kufanikisha malengo yake ya kulipa kisasi katika msimu huu.

 

“Tuliwakosea sana mashabiki wetu katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Yanga, nafahamu wanafurahia ubingwa lakini bado wana maumivu ya kufungwa na Yanga.

 

“Mchezo wa Simba na Yanga siyo mdogo ni mkubwa kwani upo katika nafasi ya tano katika dabi bora Afrika.

 

“Hivyo ni lazima tupate matokeo mazuri ya ushindi utakaokuwa na faida kwangu kutengeneza rekodi, kuwapa furaha mashabiki wetu,” alisema Gomes.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Leave A Reply