The House of Favourite Newspapers

Gomes Apata Dawa ya Wabotswana

0

KOCHA mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kuwa anahitaji safu yake ya ushambuliaji iweze kuwa bora ili kuweza kuamua mchezo wa kwanza wa ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy ambapo kocha huyo anaamini kuwa kama safu yake ya ushambuliaji itatumia vyema nafasi watakazopata basi wataimaliza mechi hiyo wakiwa ugenini.

 

Simba inatarajiwa kukipiga ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy ya nchini Botswana Octoba 17 katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika huku mchezo wa marejeano ukitarajiwa kufanyika Octoba 24 Dar katika Uwanja wa Mkapa.

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba ipo chini ya washambuliaji John Bocco, Meddie Kagere mwenye uraia wa Rwanda na Chris Mugalu anaetokea DR Congo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa kuelekea katika mchezo huo wanatakiwa kuiboresha safu yao ya ushambuliaji ambayo inahitaji kuwa bora na kuweza kutumia nafasi ili waweze kuamua mechi hiyo huku kocha huo akiweka wazi kuwa endapo safu yake ya hiyo ushambuliaji itakuwa makini katika kutumia nafasi wataweza kuibuka na ushindi wakiwa ugenini.

 

“Tunahitaji safu yetu ya ushambuliaji kutumia nafasi watakazozipata ili tuweze kuibuka na ushindi tukiwa ugenini,mechi za kimataifa zinahitaji utumiaji mkubwa wa nafasi,kama tutapata nafasi nyingi na tukashindwa kuzitumia basi tutajiweka katika nafasi mbaya,washambuliaji wangu wanalifahamu hilo lakini kusisitiza ni jambo muhimu kutoka kwangu kama mwalimu.

 

“Bado timu haijachanganya na wachezaji ndio wanaanza kuwa katika hali ya kuimarika,wachezaji wetu katika safu ya ushambuliaji tayari wote wamecheza katika michezo ya ligi kuu iliyopita,wapo katika ubora wao lakini naamini watakuwa bora zaidi,tunahitaji mabao mengi kutoka kwao haswa kuelekea katika mchezo wetu wa ligi ya mabingwa,muhimu kwao ni kutumia nafasi,”alisema kocha huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply