The House of Favourite Newspapers

Aibu Nzito ya Mchungaji Alawiti Watoto 13, Yamfika Mazito

0

HII ni aibu nzito kwa mchungaji na kanisa kwa jumla! Mchungaji Didas Mpagi almaarufu Pastor Bakulu yamemfika mazito maishani mwake baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti watoto wa kiume wapatao kumi na watatu (13).

 

Mahakama Kuu inayoshughulikia makosa ya jinai nchini Uganda, Ijumaa iliyopita ya Oktoba 8, 2021 ilimhukumu Bakulu kifungo cha maisha jela baada ya kumkuta na hatia ya kulawiti idadi hiyo ya watoto.

Bakulu ambaye wakati anatenda matendo hayo mwaka 2018 hadi 2019, alikuwa ni Mkuu wa Shule ya Msingi Real Infant na mchungaji huko wilayani Wakiso, Uganda.

KUKAMATWA KWA BAKULU

Jaji David Wangutusi aliiambia mahakama hiyo kuwa, Bakulu atatumikia kifungo cha maisha yake yote jela kutokana na ukubwa wa makosa aliyoyatenda.

Kukamatwa kwa mchungaji huo mwaka 2019 kulitokana na uchunguzi uliofanywa na Polisi baada kutonywa na wasamaria wema juu ya uwepo wa jambo hilo.

 

Baada ya uchunguzi, ilibainika kwamba, Bakulu hakuwa mkuu wa shule pekee, bali alikuwa amejipa pia cheo cha msimamizi wa hosteli za wanafunzi wa kiume.

Pia ilibainika kwamba, mchungaji huyo naye alikuwa akilala kwenye hosteli hizohizo za watoto wa shule ya msingi wa kiume na kutekeleza unyambilishi wake kila ilipofika usiku.

WATOTO KUTOKA FAMILIA MASKINI

Uchunguzi pia ulionesha kwamba, Bakulu alifanya hivyo hasa kwa watoto ambao walikuwa wanatoka kwenye familia duni (maskini) kwa kuwarubuni na vitu vidogovidogo ambavyo alijua hawavipati kutoka kwa familia zao kama ilivyo kwa watoto wa matajiri.

 

Kingine alikuwa akiwaahidi kuwapa udhamini wa kuwasomesha bure na kutowasumbua pale wazazi wao walipokosa au kuchelewa kulipa ada ya shule.

Upande wa mashtaka uliieleza mahakama kuwa, kwa kuwa watoto walikuwa kwenye shule na hosteli zake, Bakulu alikuwa akiwatisha kuwaondolea udhamini wa masomo na kuwarudisha makwao.

MCHEZO MZIMA ULIKUWA HIVI;

“Mmoja wa waathirika alipohojiwa na Polisi aliwaeleza kuwa ilimbidi kutumia usiku wake kwenye kitanda cha Bakulu na kila aliyeingia humo alitakiwa kulala akiwa mtupu. Alichokuwa akikifanya Bakulu ni kuanza kuwashikashika sehemu mbalimbali za miili yao na hasa sehemu za siri na kinachofuata ni kutaka wanyonye uume kisha kuwalawiti…” Upande wa mashtaka uliieleza mahakama.

 

Mahakama ilijiridhisha kuwa, Bakulu alitumia sehemu ya pesa zake kuwafanya watoto hao wa kiume kuwa watumwa wa ngono kwa kuwatengenezea hofu ya kisaikolojia na vitisho ili wasitoe taarifa kwa mtu yeyote.

Polisi walipofanya upekuzi kwenye chumba chake walikuta baadhi ya vitu vya ushahidi kama mafuta ya kujichua, mafuta ya krimu, barua za mapenzi kutoka kwa watoto hao, picha kwenye simu yake na flash na vinginevyo.

JELA KIFUNGO CHA MAISHA

Baada ya kusoma huku hiyo kwa saa kadhaa, Jaji alimhukumu Bakulu kifungo cha maisha huku akimpa siku 14 tangu Ijumaa iliyopita kwa ajili ya kukata rufaa kama hakuridhishwa na hukumu hiyo.

STORI; MWANDISHI WETU, DAR

Leave A Reply