The House of Favourite Newspapers

Gomes Ataja Siri za Kuimaliza AS Vita

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes amesema ataitumia michezo miwili ya Ligi Kuu Bara sawa na dakika 180 kukiandaa kikosi chake vema kabla ya kuwavaa wapinzani wake AS Vita ya Kinshasa Congo.

Simba, jana ilitarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa kiporo cha ligi dhidi ya Dodoma Jiji FC kabla ya kucheza na Azam FC, keshokutwa Jumapili.

 

Timu hiyo mara baada ya kucheza michezo hiyo miwili, Jumatano inatarajiwa kuanza safari ya Jumatano ijayo kuelekea Congo kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Gomes alisema kuwa ataitumia vema michezo hiyo miwili ya ligi kama sehemu ya maandalizi katika mchezo huo wa kimataifa.

Gomes alisema kuwa michezo hiyo ya ligi itamsaidia kukipata kikosi cha kwanza atakachokitumia katika mchezo dhidi ya Vita, hivyo ni lazima wapate matokeo mazuri ili kutengeneza hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.

 

Aliongeza kuwa wanafahamu wana ratiba ngumu, lakini hiyo hataki iwe sababu ya kupoteza michezo hiyo miwili ya ligi na huo wa kimataifa watakaoucheza.“Nimefanya kikao na wachezaji wangu na kikubwa nimewataka kila mmoja kujibidiisha wakiwa uwanjani pamoja kucheza kwa tahadhari michezo yote miwili dhidi ya Dodoma Jiji na Azam ambazo zote ngumu.“

Lengo likiwa ni kuepuka kupata majeraha yatakayowasababishia kuukosa mchezo wetu wa kimataifa dhidi ya Vita, ninaamini watazingatia maagizo yangu na kufuata kile ambacho nakitaka.

 

“Kikubwa ninataka kupata matokeo mazuri ya ushindi katika michezo hii miwili ya ligi kwa lengo la kupunguza idadi ya pointi ambazo wapinzani wetu Yanga wametuongoza,” alisema Gomes.

AISHI MANULA na BOCCO Watajwa BUNGENI Leo, HOTUBA ya RAIS MAGUFULI IKIJADILIWA

 

Leave A Reply